Wananchi wajichanganya mpango wa Serikali kuwapima afya bure

Picha ya Maktaba.

Muktasari:

  • Mpango wa Serikali ni kupima wananchi afya kwa wale ambao hawajawahi kufanya hivyo.
  • Matangazo yamekuwa yakitolewa eneo la viwanja vya Mnazi Mmoja kuwa walioleta wagonjwa wawarudishe huku wengine wakikata tamaa na kuamua kuondoka.

Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wameshindwa kuelewa mpango wa Serikali kupima wananchi afya jijini Dar es Salaam na kuleta wagonjwa kutoka hospitalini.

Mpango wa Serikali ni kupima wananchi afya kwa wale ambao hawajawahi kufanya hivyo.

Matangazo yamekuwa yakitolewa eneo la viwanja vya Mnazi Mmoja kuwa walioleta wagonjwa wawarudishe huku wengine wakikata tamaa na kuamua kuondoka.

Mmoja wa waliokuja kucheki afya, Wallace Gumbo mkazi wa Dunda anasema alijihimu kufika saa 11 alfajiri lakini amekata tamaa baada ya kukuta umati mkubwa