Wanandoa wafariki wakipishana kwa saa moja

Muktasari:

Ndugu wa wanandoa hao walizungumza na vyombo vya habari likiwamo gazeti la mtandaoni la Daily Mail.

Wanandoa wawili katika jimbo la Illinois, waliokuwa wameoana kwa miaka 69, wamefariki wakipishana kwa saa moja pekee.

Ndugu wa wanandoa hao walizungumza na vyombo vya habari likiwamo gazeti la mtandaoni la Daily Mail.

Isaac Vatkin, 91, alikata roho akiwa amemshika mkono mkewe Teresa, 89.

Gazeti la Daily Herald limeripoti kuwa Isaac alifariki kwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu. Teresa alifariki dakika 40 baadaye.

Jamaa zao walisema walifarijiwa kwamba wawili hao walikuwa pamoja hadi mwisho.

"Tusingelipenda kuwaona wakituacha," alisema mjukuu William Vatkin

"Upendo wao kwa kila mmoja ulikuwa mkubwa sana, mmoja wao hangeweza kuishi bila mwenzake," binti yao Clara Gesklin alisema wakati wa mazishi yao.

"Walipendana sana, hadi mwisho. Hadi sekunde ya mwisho," alisema Rabbi Barry Schechter, aliyeongoza ibada ya wafu katika eneo la Arlington Heights, viungani mwa mji wa Chicago.

Wanandoa hao walikuwa na watoto watatu ambao waliwalea katika eneo la Skokie, Illinois.

Isaac alikuwa mwuzaji nyama na Teresa  alikuwa akifanya shughuli za kupamba nyumba na kuwatengeneza wanawake  mikono na kucha.