Wanaokiuka haki za binadamu kufikishwa mahakamani

Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa Palamagamba Kabudi 

Muktasari:

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Wa Rais, Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa Palamagamba Kabudi amesema hayo wakati wa maadhimisho ya nne  ya Siku ya Watetezi wa haki za Binadamu chini ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC) na kuhusisha wadau kutoka asasi za kiraia,Serikalini na mashirika ya kimataifa.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuheshimiwa nchini,Serikali imesema itachukua hatua stahiki kukabiliana na wakiukaji wa haki hizo ikiwamo kuwafikisha mahakamani.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Wa Rais, Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa Palamagamba Kabudi amesema hayo wakati wa maadhimisho ya nne  ya Siku ya Watetezi wa haki za Binadamu chini ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC) na kuhusisha wadau kutoka asasi za kiraia,Serikalini na mashirika ya kimataifa.

Profesa Kabudi amesema hatua nyinginezo ni kutunga sheria za kuwalinda watetezi Wa haki za binadamu pamoja na kuridhia mikataba ya kimataifa na kikanda ili kuimarisha ulinzi wa haki hizo.

"Serikali inasimamia na kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinaheshimiwa.Asasi za kiraia,vyombo vya habari na wadau wengine wanaweza kuchukua hatua stahiki katika kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu Sheria na sera,"alisema Profesa Kabudi.

Maadhimisho hayo, yamelenga kuimarisha uhusiano kati ya watetezi wa haki za binadamu na Serikali ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuzindua ripoti ya hali ya utetezi Wa haki hizo ya mwaka 2016.