Wanasayansi watengeneza tumbo la uzazi la bandia

Muktasari:

Kifaa hicho ambacho kipo katika mfumo wa tumbo kimejaribiwa kwa mimba ya kondoo.

Marekani. Wanasayansi nchini Marekani wamebuni tumbo la bandia lililotengenezwa maabara  kwa ajili  ya kuwahifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao, maarufu kama njiti.

Kifaa hicho ambacho kipo katika mfumo wa tumbo kimejaribiwa kwa mimba ya kondoo.

Watafiti katika hospitali ya watoto ya Philadephia wanasema lengo lao ni kuweka mazingira ambayo watoto wanaozaliwa kabla muda wao kutimia wanaweza kukuza viungo vyao vya mwilini kama vile mapafu na viungo vyengine.

Kifaa hicho kimetengezwa kwa kutumia mfuko wa plastiki, uliojazwa maji ya kutengeza(amniotic fluid) yanayosaidia kumlinda mtoto ili kuweka mfanano na  mazingira ya tumbo la uzazi.

Wanasayansi wanaamini mfuko huo unaweza kuwa tayari kwa majaribio ya binadamu baada ya miaka mitatu mpaka mitano kuanzia sasa.