Wanaume hujinyonga wakishindwa kuvumilia aibu-Mtaalamu

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa saikolojia katika Chuo cha Ualimu Patandi, Tawi la Sahare Tanga, Modesta Kamoga alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tukio la mfanyabiashara Mohammed Mohammed (46) mkazi wa Dar es Salaam kumuua mkewe, Sophia na kisha kujinyonga.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa wanawake wanauwezo mkubwa zaidi wa kuvumilia wanapopatwa na aibu kuliko wanaume ambao baadhi yao huamua kujinyonga.

Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa saikolojia katika Chuo cha Ualimu Patandi, Tawi la Sahare Tanga, Modesta Kamoga alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tukio la mfanyabiashara Mohammed Mohammed (46) mkazi wa Dar es Salaam kumuua mkewe, Sophia na kisha kujinyonga.

Mohammed alimuua mkewe na kuacha ujumbe wenye kurasa 80 ukieleza sababu za kufanya tukio hilo, kubwa ikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi wa muda mrefu.

 “Wanaume wanapokumbwa na aibu kubwa kama huyo mtu aliyegundua kuwa watoto siyo wa kwake. Angekuwa mwanamke akajua mumewe ana watoto nje ya ndoa, anakwenda kumwambia mtu wake wa karibu, wanaume hawawezi kutoa sumu moyoni,” alisema.