Wanawake kuchunguzwa majeraha

Muktasari:

Uchunguzi huo utafanywa na Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la WomenforWomen kutoka Marekani.

Dar es Salaam. Wanawake na wasichana wasiopungua 250,  Oktoba 29 watafanyiwa uchunguzi wa majeraha ya viungo kutokana na ulemavu na ngozi.

Uchunguzi huo utafanywa na Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la WomenforWomen kutoka Marekani.

Meneja Miradi wa Aga Khan, Nasreen Hassanali amesema jana kuwa watakaobainika kuathirika zaidi na ulemavu wa viungo na ngozi uliotokana na majanga ya moto na ajali watafanyiwa upasuaji bure kurekebisha sehemu hizo.

Alisema kambi ya uchunguzi itafanyika katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana itakayoongozwa na daktari bingwa, Edwin Mrema.