Wanawake wafugaji waonyesha hasira zao

Muktasari:

  • Wakizungumza juzi eneo hilo, wanawake hao walidai kuwa kilimo cha vitunguu kikiachiwa kiendelee pembeni mwa ziwa hilo, kutawaathiri wananchi wa kata za Bassotu na Mulbadaw, ambao shughuli zao za kila siku zinategemea maji hayo.

Hanang’. Wanawake wa jamii ya wafugaji wa Kidatoga wa Tarafa ya Bassotu wilayani Hanang, wamezuia kilimo cha umwagiliaji cha vitunguu kwenye Ziwa Bassotu wakidai kinasababisha ziwa hilo kukauka.

Wakizungumza juzi eneo hilo, wanawake hao walidai kuwa kilimo cha vitunguu kikiachiwa kiendelee pembeni mwa ziwa hilo, kutawaathiri wananchi wa kata za Bassotu na Mulbadaw, ambao shughuli zao za kila siku zinategemea maji hayo.

Mmoja wa wanawake hao, Helena Bajuta alisema wao ni wana mazingira wanaosimama kidete kuhakikisha Ziwa Bassotu linaheshimiwa na jamii ya eneo hilo,  pia linaendelea kutunzwa ili waendelee kulitumia wao na vizazi vijavyo.

Ofisa Tarafa ya Bassotu, Jeremiah Mhangaza alisema wote ambao wameharibiwa mazao yao na wanawake hao, wanatakiwa kufika kwenye vyombo vya sheria ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao.