Wanawake wamwomba Magufuli arudi kwenye meza ya mazungumzo

Rais John Magufuli

Muktasari:

Akizungumza na wanahabari jana, mratibu wa wanawake wa UMD, Mwajuma Noty alisema chokochoko zinazoendelea zikiachwa bila kukemewa, urithi wa tunu ya amani unaweza kupotea na nchi kuingia kwenye machafuko.

Dar es Salaam. Viongozi wanawake wa vyama vya siasa vya Ada-Tadea, UMD na Demokrasia Makini, wamemuomba Rais John Magufuli kufanya kikao cha haraka na viongozi wa kisiasa kujadili hali inayoendelea nchini, hususan operesheni Ukuta.

Akizungumza na wanahabari jana, mratibu wa wanawake wa UMD, Mwajuma Noty alisema chokochoko zinazoendelea zikiachwa bila kukemewa, urithi wa tunu ya amani unaweza kupotea na nchi kuingia kwenye machafuko.

Alisema njia inayotumiwa na Chadema kudai haki ya kidemokrasia ni ya hatari licha ya kwamba hakuna chama kinachokubaliana na kauli ya Rais kupiga marufuku siasa hadi ifikapo mwaka 2020.

“Siku zote katika siasa kumalizika kwa uchaguzi ndio mwanzo wa siasa,” alisema.