Waomba adhabu ya viboko irudishwe

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Msichana Initiative unaotekelezwa na asasi ya Fadhili Teens Tanzania katika Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kamanga B, Gamba Maregesi alisema vijana wanapokemewa wazazi huja juu.

Serikali imeombwa kurudisha utaratibu wa zamani wa kumwadhibu mtoto kwa kumchapa viboko anapokuwa ametenda kosa bila kupata ridhaa ya mzazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Msichana Initiative unaotekelezwa na asasi ya Fadhili Teens Tanzania katika Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kamanga B, Gamba Maregesi alisema vijana wanapokemewa wazazi huja juu.

“Vijana wanafanya makosa lakini wanapokemewa na kuadhibiwa wazazi huja juu, tofauti na ilivyokuwa zamani mzazi kumpa adhabu hata mtoto wa jirani yake bila kuulizwa.”

Msimamizi wa mradi huo, Eminaely Tibesigwa, alisema lengo la mradi huo ni kuwasaidia wasichana ili kufikia ndoto zao baada ya kubaini kuwa asilimia kubwa wanaharibikiwa maisha kutokana na changamoto lukuki zikiwamo za kubeba ujauzito wakiwana umri mdogo. (Mwandishi Wetu)