Wapangaji TBA Dodoma mguu ndani mguu nje

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga.

Muktasari:

Hata hivyo, bado Serikali haijaridhia uamuzi huo wa kuhamisha wapangaji hao.

Dar es Salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imesema italazimika kuwahamisha baadhi ya wapangaji katika nyumba zake ili zikaliwe makatibu wa wizara mjini Dodoma.

Hata hivyo, bado Serikali haijaridhia uamuzi huo wa kuhamisha wapangaji hao.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga.

Pia, alisema TBA imepewa jukumu la kuandaa majengo ya ofisi na makazi mkoani humo kwa ajili ya viongozi, na watumishi wa Serikali wanaotakiwa  kuhamia huko.

Mwakalinga alisema kutokana na unyeti wa jukumu hilo, wamejipanga na kuanza kulifanyia kazi kwa kufanya tathimini ya majengo ambayo yatatumika kwa ofisi na mengine ya makazi ya kuishi.