Wapinzani, Maalim Seif lao moja

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Muktasari:

Aboud alitoa tamko hilo siku moja baada ya Umoja wa Vijana wa CCM kulaumu mwenendo huo wa Maalim Seif, uliodai kiongozi huyo anakwenda kinyume kwa kuhubiri siasa katika nyumba za ibada.

Zanzibar. Baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed kumkataza Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuzungumza misikitini kwa kuwa anakiuka utaratibu, Vyama vya siasa vimepinga tamko hilo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Aboud alitoa tamko hilo siku moja baada ya Umoja wa Vijana wa CCM kulaumu mwenendo huo wa Maalim Seif, uliodai kiongozi huyo anakwenda kinyume kwa kuhubiri siasa katika nyumba za ibada.

Baadhi ya viongozi wa vyama siasa vya upinzani walipinga uamuzi wa Serikali wa kumzuia Maalim Seif huku upande wa chama tawala, CCM ukiunga mkono.

Katibu Mkuu wa Jahazi Asilia, Haji Mtumweni amesema: “Kauli ya Mohamed Aboud haipaswi kutolea uamuzi bila ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya kile anachoendelea nacho Maalim Seif.”