Wasanii 400 kupamba Sauti za Busara

Muktasari:

Tamasha hilo   lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ kwa mara ya kwanza mwaka huu  majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa na nyumbani.

Jumla ya wasanii 400 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la kimataifa la Sauti za busara litakaloanza kurindima Februari 9 hadi 12 mwaka huu.

Tamasha hilo  lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ kwa mara ya kwanza mwaka huu  majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa na nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya mawasiliano ya Busara Music wasanii hao watakuwa ndani ya makundi 40 ambayo yatatumbuiza ‘live’ jukwaani.

Makundi hayo ni Afrijam Band, CAC Fusion, Chibite Zawose Family, Cocodo African Music Band, Jagwa Music, Matona's G Clef Band, Mswanu Gogo Vibes, Rajab Suleiman & Kithara, Tausi Women's Taarab, Usambara Sanaa Group, Wahapahapa Band na Ze Spirits Band.

Mengine ni  Batimbo Percussion Magique (Burundi), Bob Maghrib (Morocco), Buganda Music Ensemble (Uganda), Grace Barbe (Seychelles), H_art the Band (Kenya), Imena Cultural Troupe (Rwanda), Isau Meneses (Mozambique) na Karyna Gomes (Guine Bissau),

Jukwaa litashambuliwa pia na Kyekyeku (Ghana), Loryzine (Reunion), Madalitso Band (Malawi), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Rocky Dawuni (Ghana), Roland Tchakounté (Cameroon), Sahra Halgan Trio (Somaliland), Sami Dan and Zewd Band (Ethiopia), Sarabi (Kenya), Simba & Milton Gulli (Mozambique).