Wasilisheni michango ya maafa mapema- Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Muktasari:

Amesema jana kuwa Serikali ilianza kugawa misaada hiyo kwa waathirika wa nyumba zilizoanguka, kwa kuanza kujengwa upya na Jeshi la Wananchi (JWTZ) lipo huko kwa ajili ya kusaidia kazi hiyo

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi na walioahidi kuchangia maafa baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani Kagera kuwasilisha michango hiyo mapema.

Amesema jana kuwa Serikali ilianza kugawa misaada hiyo kwa waathirika wa nyumba zilizoanguka, kwa kuanza kujengwa upya na Jeshi la Wananchi (JWTZ) lipo huko kwa ajili ya kusaidia kazi hiyo.

Majaliwa amesema hayo baada ya kupokea msaada wa Sh40 milioni kutoka Jukwaa la Wafanyabiashara wa India walioko nchini (IBF) na Kampuni ya Ujenzi ya China (Chico), kila moja ikichangia Sh20 milioni.

Tetemeko la ardhi hilo lilisababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, uharibifu wa nyumba 2,063 na nyingine 14,081 kuwa katika hali hatarishi.