Wasomali washindwa kuchagua bunge jipya

Muktasari:

Takriban wajumbe 14,000 walistahili kuchagua bunge la juu na la chini mwishoni mwa wiki lakini hata hivyo hakuna kura iliyopigwa.

Mchakato wa kuchagua bunge jipya nchini Somalia umeahirishwa.

Takriban wajumbe 14,000 walistahili kuchagua bunge la juu na la chini mwishoni mwa wiki lakini hata hivyo hakuna kura iliyopigwa.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa itaathiri uchaguzi wa Urais wa nchini humo.

Hakuna sababu iliyotolewa, lakini ripoti kutoka nchini Somalia zinasema kuwa kuna tofauti ambazo hazijatatuliwa kuhusu ni vipi mchakato huo utakavyoendeshwa.

Mipango ya watu kupiga kura ilitupiliwa mbali kutokana na ukosefu wa usalama na miundo msingi.

Mabunge hayo mawili yanastahili kumchagua rais ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao.

Vilevile uchaguzi wa urais utafanyika mwezi Novemba tarehe 30.