Wataka maofisa polisi wawajibishwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa

Muktasari:

Maofisa hao, mmoja akiwa na cheo cha Mrakibu wa Polisi (ASP) na mwingine  Koplo, walikamatwa na magari matatu ya wizi ambayo yalisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.

Moshi. Wakazi wa mji wa Himo wilayani Moshi, wamehoji hatua ya polisi kutowawajibisha maofisa wake wawili wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa magari.

Maofisa hao, mmoja akiwa na cheo cha Mrakibu wa Polisi (ASP) na mwingine  Koplo, walikamatwa na magari matatu ya wizi ambayo yalisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya Polisi, zinadai maofisa hao walikamatwa na magari hayo mwezi uliopita na kikosi kazi maalumu kutoka  Dar es Salaam, lakini hadi sasa  wapo kazini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amekiri maofisa wake kukutwa na magari hayo, lakini akasema mtu hawezi kupewa adhabu kabla ya kuthibitika kuwa kafanya uhalifu.