Dk Magufuli: Watakaong’ang’ania kubaki Dar wamejifukuzisha kazi

Rais John Magufuli 

Muktasari:

Alitoa msimamo huo mjini hapa jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara mkoani Singida tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.

Singida. Rais John Magufuli amesema azma ya Serikali yake kuhamia Dodoma haraka iwezekanavyo ipo pale pale huku akiwaonya wale wataong'ang'ania kubaki Dar es Salaaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

Alitoa msimamo huo mjini hapa jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara mkoani Singida tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.

Alisema kuwa licha ya kuhamia Dodoma atahakikisha anauza majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam kwa mnada ili wale wasiotaka kuhama,wahame kwa lazima.