Watano wahukumiwa kunyongwa kesi ya bilionea Msuya


Muktasari:

  • Mahakama imemwachia huru mshitakiwa wa pili baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake


Moshi. Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua kwa makusudi mfanyabiashara wa Arusha na Mirerani, Erasto Msuya.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni mshitakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed; mshitakiwa wa tatu, Mussa Mangu; wa tano, Karim Kuhundwa; wa sita Sadick Mohamed na wa saba; Ally Mussa Majeshi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 23, 2018 na Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo.

Pia, Mahakama imemwachia huru mshitakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

Soma zaidi: