Watatu wauawa kwa risasi

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro

Muktasari:

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema tukio hilo lilitokea jana eneo la Mikocheni karibu na Shule ya Sekondari ya Feza ambako jeshi hilo liliweka mtego baada ya kupewa taarifa za kuwapo mpango wa kufanyika uhalifu.

Dar es Salaam. Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi  baada ya kuwapo kwa taarifa za kutaka kuvamia Jengo la Bima, Mikocheni jijini hapa.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema tukio hilo lilitokea jana eneo la Mikocheni karibu na Shule ya Sekondari ya Feza ambako jeshi hilo liliweka mtego baada ya kupewa taarifa za kuwapo mpango wa kufanyika uhalifu.

Sirro amesema baada ya kupewa taarifa hizo, walikwenda kwenye eneo la tukio na walipofika walianza kurusha risasi za moto hewani, ndipo majambazi hao walipojibu na kuanza kujibizana kwa silaha.

“Ni kweli majambazi watatu wameuawa na mmoja amekimbia na pikipiki waliyokuwa wakiitumia. Jeshi la polisi tunaendelea kumtafuta,” amesema Sirro.