Watoto waanza kushuka kwenye ndege

Wanafunzi watatu na wajumbe 16 wa shirika la Samaritan kutoka Marekani wamewasili asubuhi hii Uwanja wa KIA wakiwasindikiza watoto watatu wa shule ya Lucky Vincent.

Wajumbe hao pia wamelakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Anna Mghwira ambaye ameongoza wakazi wa mkoa huo kuwapokea wanafunzi hao.

 Wanafunzi waliorejea ni Doreen Mshana,Sadia Awadh na Wilson Tarimo

Wanafunzi hao ni manusura wa ajali iliyotokea mwezi wa tano wamelakiwa na umati wa watu wakiwamo Wanafunzi wenzao wa  shule ya Lucky Vicent.