VIDEO: Watu 20 wafariki dunia ajali ya magari manne

Muktasari:

Kazi ya uokoaji ilishirikisha vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 

Mbeya. Watu 20 wamekufa papo hapo na wengine 45 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea Mlima Iwambi wilayani Mbeya.

Ajali hiyo iliyotokea leo Julai Mosi, 2018 imehusisha magari manne zikiwamo daladala tatu na lori moja.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu ametoa taarifa hiyo baada ya kazi ya uokoaji kukamilika.

Wananchi wakishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walishiriki katika uokoaji. Moja kati ya daladala hizo lililaliwa na lori.

Lori liliyagonga magari hayo yaliyokuwa yakitokea stendi ya Mbalizi kuelekea Mbeya mjini.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alikuwapo eneo la tukio ambako kazi ya uokoaji ilishirikisha vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).