Watumishi wa umma washauriwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi (WHC), Dk Fred Msemwa .

Muktasari:

  • Ushauri huo, ulitolewa leo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi (WHC), Dk Fred Msemwa wakati akizungumza na wanahabari juu ya mpango wa taasisi hiyo  kujenga nyumba katika mji wa Dodoma .

Dar es Salaam.Watumishi wa umma na Watanzania wameshauriwa kununua nyumba zinazouzwa na taasisi mbalimbali ili kuokoa gharama kubwa pindi wanapoamua kujenga wenyewe.

Ushauri huo, ulitolewa leo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi (WHC), Dk Fred Msemwa wakati akizungumza na wanahabari juu ya mpango wa taasisi hiyo  kujenga nyumba katika mji wa Dodoma .

Alisema utafiti mdogo alioufanya amebaini kuwa Watanzania na watumishi wa umma wanatumia gharama kubwa katika ujenzi wa nyumba kutokana na mazingira wanayoishi.

Alisema baadhi ya watumishi wamechukua viwanja  na wengine wana nyumba lakini hawajaziendeleza na ujenzi wao umekuwa ukichukua miaka miwili hadi 15

"Mfano mtu kapanga , wakati huohuo anajenga nyumba kwa miaka Halafu muda huo anatakiwa kulipa pango la nyumba anakoishi," alisema Dk Msemwa.