Wavamia kituo cha polisi wakimtaka Sangoma wao

Kamanda  wa Polisi Tanga, Benedict Wakulyamba.

Muktasari:

  • Polisi ililazimika kupiga mabomu ya machozi  angani ili kutawanya kundi la watu hao waliovamia kituo cha polisi wakishinikiza kuachiwa kwa sangoma huyo  huku wakifanya vurugu, wakidai mganga hiyo ni muhimu katika kijiji chao.

Tanga. Watu kadhaa wametiwa nguvuni na jeshi la polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga asubuhi hii baada ya kundi la wakazi wa Kijiji cha Mgombezi kuandamana  wakidai kuachiwa huru kwa sangoma aliyedaiwa na wakazi hao kusaidia kuondoa wachawi.

Polisi ililazimika kupiga mabomu ya machozi  angani ili kutawanya kundi la watu hao waliovamia kituo cha polisi wakishinikiza kuachiwa kwa sangoma huyo  huku wakifanya vurugu, wakidai mganga hiyo ni muhimu katika kijiji chao.

Urushaji wa mabomu hayo ya machozi ulisababisha watu kadhaa kukamatwa na jeshi hilo wakitutuhumiwa kufanya maandamano haramu.

Hali hiyo imesababisha shughuli za kawaida  na usafiri katika kituo cha mabasi cha Korogwe kilicho jirani na kituo hicho cha polisi kusimama kwa muda huku wasafiri  na wafanyabiashara wakitimua mbio.