Wavuvi wagoma kutumia nyavu zenye matundu 26

Muktasari:

Wakizungumza na gazeti hili juzi, baadhi ya wavuvi hao walisema tangu mwaka 2000 walikuwa wanaruhusiwa kutumia nyavu zenye matundu 78.

Mwanza. Zaidi ya wavuvi 2,000 katika Mwalo wa Igombe, Wilaya ya Ilemela  mkoani hapa wamegoma wakipinga agizo la Serikali la kuwataka kutumia nyavu zenye matundu 26, badala ya 78.

Wakizungumza na gazeti hili juzi, baadhi ya wavuvi hao walisema tangu mwaka 2000 walikuwa wanaruhusiwa kutumia nyavu zenye matundu 78.

“Tumelazimika kusimamisha zaidi ya  mitumbwi 320 kufuatia agizo la Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alilolitoa kwa wavuvi wa sangara, kututaka tusitumie nyavu zenye matundu 78,” alisema Paul James, mmoja wa wavuvi hao.

Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu), Frank Mwakimonga alisema uvuvi wa kutumia nyavu zenye matundu 78 unafaa kwa wavuvi kwa sababu huwarahishia kuvua samaki kwenye kina kirefu cha maji na hutumia nyenzo za kisasa.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi