Wazabuni watangaziwa kiama

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kibaha Mkoani  Pwani, Tatu Selemani

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Selemani  alisema hayo juzi baada ya kuhitimisha  ziara ya  siku moja ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliyofanya wilayani hapa ili kuona utekelezaji wa miradi.

Pwani. Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, itaendelea kuongeza umakini katika utoaji zabuni kwa wanaoomba kazi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

 Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Selemani  alisema hayo juzi baada ya kuhitimisha  ziara ya  siku moja ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliyofanya wilayani hapa ili kuona utekelezaji wa miradi.

“Tunataka miradi yote itakayokuwa kwenye bajeti itekelezwe kwa wakati ili kuleta manufaa kwa wananchi wetu, hivyo hatutakuwa tayari kumpa zabuni atakayeonekana anafanya kazi kwa ubabaishaji.

“Ni lazima tujiridhishe kuwa ana mtaji, sifa na weledi wa hali ya juu ndipo tumpitishie zabuni,” alisema.