Wazazi watajwa kuwa kikwazo cha udhibiti mimba za utotoni

Muktasari:

Mwirinde alisema hayo jana kwenye kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa kujadili tatizo la mimba, ubakaji na ulawiti kwa watoto wilayani Rombo.

Rombo. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Naomi Mwirinde amesema  tatizo la mimba na kulawiti watoto ni gumu kwisha kutokana na wazazi kuwakataza watoto kusema ukweli wanapofanyiwa ukatili huo.

Mwirinde alisema hayo jana kwenye kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa kujadili tatizo la mimba, ubakaji na ulawiti kwa watoto wilayani Rombo.

 Kongamano hilo lililenga kuweka mikakati itakayosaidia kutokomeza ukatili huo, ambao unaendelea kushika kasi mwaka hadi mwaka.