Wazee wa mila wachongewa

Muktasari:

Luoga alisema fedha hizo zitawasaidia wanawake hao kufanya shughuli za ujasiriamali badala ya kutegemea ukeketaji.

Tarime. Hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga kuagiza fedha za Serikali zitakazokwenda vijijini kwa ajili ya maendeleo, kutolewa kiasi kuwakopesha mangariba ili waongezee mitaji ya biashara, imesababisha wanawake hao kuwachongea wazee wa mila.

Luoga alisema fedha hizo zitawasaidia wanawake hao kufanya shughuli za ujasiriamali badala ya kutegemea ukeketaji.

Mangariba wanaojihusisha na kukeketa wasichana wilayani hapa Mkoa wa Mara, waliitaka Serikali kuwakamata wazee wa kimila kwani ndiyo chanzo cha wao kufanya kazi hiyo kwa kulazimishwa.

Akizungumza juzi, mkazi wa Kijiji cha Mriba aliyekuwa ngariba, alidai kuwa wazee hao huwafuata  nyumbani kwao na kuwalazimisha wawakekete wasichana wanaowapeleka na wakikataa, huwatishia kuwadhuru.

Alisema ameamua kuachana na kazi hiyo kwa sababu ina madhara makubwa kwa wasichana na familia zao.  Mangariba 68 walipata mafunzo ya ujasiriamali.