Waziri Castico awafunda watetezi wa haki za watoto

Waziri wa kazi, vijana, wanawake, wazee na watoto, Moudline Castico

Muktasari:

Waziri wa kazi, vijana, wanawake, wazee na watoto, Moudline Castico alitoa kauli hiyo juzi Malindi mjini Unguja katika uzinduzi wa mafunzo kwa wadau wa utetezi wa haki za watoto.

Zanzibar. Watetezi wa haki za watoto nchini, wametakiwa kuacha jazba katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuhakikisha watoto wanapata haki zao bila ya usumbufu.

Waziri wa kazi, vijana, wanawake, wazee na watoto, Moudline Castico alitoa kauli hiyo juzi Malindi mjini Unguja katika uzinduzi wa mafunzo kwa wadau wa utetezi wa haki za watoto.

Casticoalisema ili kufanikisha upatikanaji suluhu au haki za watoto kisheria, lazima watetezi kutumia lugha nzuri ambayo itakuwa rafiki na chanzo cha kupata haki inayotafutwa.

Alisema utumiaji wa maneno ya jaziba mara nyingi hayasaidii wala hayawezi kufanikisha upatikanaji wa haki za watoto.

Naye mratibu wa mtandao wa haki za watoto Tanzania, Onesmo Ole Ngurumwa alisema ni vyema kwa wafuatiliaji haki za watoto kwanza wajifunze sheria za nchi kuhusu mtoto badala ya kujiingiza katika kazi hiyo kwa kukurupuka.