Waziri Makamba ashiriki upandaji miti Iringa

Muktasari:

Katika zoezi hilo, Makamba ameongozana na mkuu wa mkoa huo, Amina Masenza, mkuu wa wilaya Iringa Mjini, Richard Kasesera na viongozi wengine wa kitaifa.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ameshiriki upandaji miti katika shule ya msingi Mlandege mkoani Iringa na kusema wanafunzi wanapaswa kushirikishwa katika mchakato huo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Katika zoezi hilo, Makamba ameongozana na mkuu wa mkoa huo, Amina Masenza, mkuu wa wilaya Iringa Mjini, Richard Kasesera na viongozi wengine wa kitaifa.

Amesema ni vyema wanafunzi  wakashirikisha katika ngazi hiyo ili kujifunza zaidi namna bora ya utunzaji wa mazingira itakayosaidia nchi kuwa katika hali nzuri.

Mkuu wa mkoa huo, Amina Masema amewataka wanafunzi na walimu wa Mlandege kuitunza miti hiyo katika hali nzuri na atakuwa akipita mara kwa mara kuikagua.

 Kwa habari zaidi nunua Mwananchi kesho au soma kwa mtandao kwa kujisajili Bonyeza Hapa