Waziri Makamba ataka Mbeya ifufue mashamba ya misitu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba

Muktasari:

Waziri Makamba amesema hayo leo alipokutana na uongozi jiji hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua uharibifu wa mazingira katika mikoa mbalimbali.

Mbeya.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ameugiza uongozi wa Mbeya kufufua mradi wa mashamba ya misitu ya nishati ili kuhifadhi mazingira yanayosababisha na ukataji wa miti hovyo.

Waziri Makamba amesema hayo leo alipokutana na uongozi jiji hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua uharibifu wa mazingira katika mikoa mbalimbali.

Katibu Tawala wa Mbeya, Mariam Mtunguja alimweleza Makamba mpango ulikuwapo hapo awali lakini ulikufa kwa sababu mbalimbali ikiwamo watu kuvamia eneo lililotengwa kwa ajili ya mrado huo.

Makamba amesema mashamba hayo yakianzishwa watu wa mkoa huo wataondoka na tabia ya kukata miti hovyo kwa ajili ya nishati ya mkaa badala ya miti itatoka katika mashamba hayo maalumu.