Waziri Mkuu Korea aondoka Tanzania

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpungia mkono mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon kabla ya kupanda ndege na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara ya siku tatu nchini. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Muktasari:

Akamilisha ziara ya siku tatu


Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yon ameondoka nchini leo baada ya kumaliza ziara yake.

Lee aliwasili juzi Julai 21, 2018 usiku kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameondoka mchana wa leo Julai 23, 2018 baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA), Lee ameagwa na mwenyeji wake, Majaliwa, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa.

Wengine waliokuwapo uwanjani ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya.

Lee baada ya kuagana na Majaliwa na viongozi wengine saa 8:50 mchana, alipanda ngazi za ndege na kuwapungia mikono na akionyesha ishara ya shukuran kwa Watanzania.