Waziri Mkuu Majaliwa akerwa msongamano wodi ya wazazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Muktasari:

Ziara hiyo ilitokana na taarifa alizolalamikiwa na wananchi juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwamba hospitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wachanga.

Arusha. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ambako kulikuwa na tuhuma za kuibwa watoto, lakini alishuhudia wazazi watatu wakilala kitanda kimoja.

Ziara hiyo ilitokana na taarifa alizolalamikiwa na wananchi juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwamba hospitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wachanga.

Hata hivyo, jana baada ya kufika katika hospitali hiyo, Majaliwa alishuhudia msongamano katika wodi ya wazazi  na kuagiza kuboreshwa hospitali za pembezoni.

Habari zaidi soma gazeti la Mwananchi