Waziri Mkuu amtaka mbunge akutane na mawaziri wawili

Muktasari:

Waziri Mkuu amemtaka Upendo Peneza azungumze na Waziri wa Fedha na wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Upendo Peneza kukutana na Waziri wa Fedha na wa Tamisemi ili kushauriana namna  bora ya kuhakikisha taulo za kike zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu ili wanafunzi wa kike wanaoshindwa kwenda shule wakati wa hedhi, wamudu kuzinunua.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 19, 2018 katika kipindi cha maswali ya hapo kwa papo kwa Waziri Mkuu baada ya mbunge huyo kumuuliza kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni kwanini Serikali katika Sheria ya Fedha ijayo isiondoe kodi katika taulo za kike ili zipatikane kwa urahisi.

Peneza amesema pedi hizo zikipatikana kwa urahisi  hakuna mwanafunzi atakayekatiza masomo kwa kukosa taulo hizo.

Peneza alisema baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini wanashindwa kumudu kununua taulo hizo na hivyo kukosa masomo.