Waziri Mkuu amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa wakuu wa nchi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

Waziri Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, John Pombe Magufuli.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Nairobi, Kenya kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa Sita wa Wakuu wa Nchi wa TICAD (TICAD VI) utakaofanyika Agosti 27 -28, mwaka huu.

Waziri Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, John Pombe Magufuli.

Leo asubuhi  Waziri Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya kibiashara kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo.

Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation, Tadashi Izawa ambapo katika mazungumzo yao, pamoja na kuangalia fursa nyingine katika sekta ya gesi Tanzania, kampuni hiyo imekubali kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa wataalamu kwa sekta ya gesi hususan usindikaji wa gesi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi (Liquefied Natural Gas).

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato na kujadiliana mambo kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.