Friday, April 21, 2017

Waziri Mkuu aongoza mamia kuuaga mwili wa Elly Macha

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameungana na wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

Akizungumza leo  katika viwanja vya Bunge, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.

Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dk Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.

-->