Waziri Mkuu kuzindua meli mbili za mizigo kesho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 

Muktasari:

Ujenzi wa meli moja ya abiria umefikia asilimia 50 na unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu.

Mbeya. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Jumamosi Julai 29, anatarajia kuzindua meli kubwa mbili za mizigo katika Bandari ya Kyela, Ziwa Nyasa jijini hapa zilizojengwa kwa gharama ya Sh11bilioni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Julai 28, Kaimu Mkuu wa Bandari ya Kyela, Ajuaye Msese amesema ujenzi wa meli hizo ambao mradi wake ulianza Juni 2015 umekamilika  na taratibu nyingine zinaendelea kabla hazijaanza kufanya kazi.
Amesema meli hizo zina uwezo wa kubeba tani 1000 za mizigo na kwamba kuna makampuni ambayo yanasubiria meli hizo kwa ajili ya kusafirisha mizigo yao ikiwa ni pamoja na Kiwanda cha Saruji Mbeya, kampuni zilizopo nchini Malawi zinazotarajia kuingiza na kutoa nafaka kupitia meli hizo.