Thursday, July 13, 2017

Waziri Zanzibar ashauri siku za Sabasaba ziwe 16

Wananchi wakiangalia mbegu za nafaka

Wananchi wakiangalia mbegu za nafaka zinazozalishwa katika mashamba ya Magereza walipotembelea Banda la Magereza kwenye Maonyesho ya 41  ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

By Kalunde Jamal, Mwananchi; kjamal@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waandaaji wa maonyesho ya biashara Sabasaba, wametakiwa kuzifanya siku 16 za maonyesho hayo kuwa za kudumu.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, Julai 13 na Waziri wa Biashara, Viwanda na masoko wa Zanzibar,   Balozi Amina Salum Ally aliyeitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) kuongeza siku za maonyesho hayo hadi 16 badala ya 11.

Balozi Ally aliunga mkono kauli iliyotolewa na Rais John Magufuli alipokuwa akifungua maonyesho hayo Julai Mosi alipoitaka Tantrade kuongeza siku tano na hivyo maonyesho hayo yaliendelea kwa siku nyingine tano hadi leo.

Kwa kawaida maonyesho ya Sabasaba humalizika Julai 8.

Balozi Ally pia ametoa wito kwa uongozi wa Tantrade kufanya tathmini ya kina kuhusu maeneo yaliyokuwa na changamoto ili yaweze kufanyiwa marekebisho.

-->