Waziri apiga marufuku ukamataji wauguzi, wakunga bila utaratibu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Muktasari:

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha uliolenga kupunguza vifo katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu, alisema wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata wauguzi,  wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha uliolenga kupunguza vifo katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu, alisema wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.

"Kumetokea baadhi ya vitendo ambavyo vinafanywa na baadhi ya viongozi wenzangu na watendaji kutoka wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya vitendo vibaya dhidi ya wauguzi na wakunga, pale ambapo muuguzi au mkunga unadhani amekosea zipo taratibu za kufuata na siyo kumweka ndani, kuna Baraza la Wakunga ambalo lina Mamlaka ya kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye amekwenda kinyume."