Wema Sepetu atinga polisi

Msanii, Wema Sepetu akiingia kituo cha Polisi

Muktasari:

Wema amewasili kituoni hapo saa 6:55 mchana akiwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Mark II.

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amefika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya zilizotolewa dhidi yake na mkuu wa mkoa, Paul Makonda.

Wema amewasili kituoni hapo saa 6:55 mchana akiwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Mark II.

Msanii huyo maarufu alikuwa amevaa gauni refu (dela) lenye maua maua na kufunga kitambaa cheusi kichwa ambacho kilificha sehemu kubwa ya uso wake.