Wema alipa faini, akwepa kifungo

Muktasari:

Wema amelipa faini hiyo leo Ijumaa Julai 20, 2018  baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kulipa faini ya Sh1milioni kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Dar es Salaam. Msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu  amelipa faini ya Sh2milioni na kuepuka kifungo cha mwaka mmoja jela.

 

Wema amelipa faini hiyo leo Ijumaa Julai 20, 2018

baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kulipa faini ya Sh1milioni kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

 

Wakati Wema akikutwa na hatia, washatakiwa wenzake ambao ni wafanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa na Matrida Abbas wameachiwa huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

 

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya dakika 45,  Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema upande wa mashtaka umeleta mashahidi watano, ambao walithibitisha mashtaka hayo.

 

Amesema baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake, washtakiwa wote walikutwa na kesi ya kujibu  na walijitetea wakiongozwa na wakili wao,  Albert Msando.

 

"Nawaachia huru mshtakiwa wa pili na wa tatu kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao lakini kwa upande wa Wema hakuna shaka lolote kwamba alipatikana na dawa za kulevya,” amesema hakimu.

 

Siku za nyuma  katika utetezi wake, Wema alikubali nyumbani kwake kulikuwa na msokoto unaodhaniwa ni bangi, vipisi ambavyo hajui ni kitu gani katika chumba cha kuhifadhia nguo zake, pochi, viatu na kibriti katika chumba wanacholala wanamuziki wawili Jordan na Mila.

 

Akiongozwa na wakili Msando kujitetea, Wema alieleza kuwa yeye hajui mmiliki wa vitu hivyo kwa sababu yeye ni msanii wa filamu na nyumbani wake wanaingia watu tofauti tofauti.

 

Amedai kawaida huwa anafanya sherehe na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mchana