Wenye vyeti feki mikononi mwa Magufuli

Muktasari:

  • Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli, kesho atapokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.

Kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba mwaka jana.