Winnie Mandela aibiwa 13milioni

Aliyekuwa mke wa Rais wa  zamani wa Afrika Kusini, Winnie Mandela

Muktasari:

Msemaji wa polisi amesema kuwa hawajamkamata mshukiwa yeyote lakini wanaendelea na uchunguzi.

Aliyekuwa mke wa Rais wa  zamani wa Afrika Kusini, Winnie Mandela ameibiwa dola 6000 (Sh 13milioni) nyumbani kwake. Polisi nchini Afrika kusini wanasema wanachunguza tukio hilo.

Msemaji wa polisi amesema kuwa hawajamkamata mshukiwa yeyote lakini wanaendelea na uchunguzi.

Mtandao wa News24 ulisema kuwa Winnie Mandela aligundua kuwa dola 6,000 ambazo alikuwa amepewa kama zawadi wakati ya sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake zilikuwa zimetoweka

Mtandao huo unasema aligundua kuwa hazikuwepo wakati alienda kutafuta pesa kumtuma mtu anunue mkate.

Ripoti zinasema kuwa alikuwa na mipango ya kuzipeleka pesa hizo kwenye benki.