Wizara yasema dawa zinapatikana kwa asilimia 53

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Mpoki Ulisubisya amesema hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi mwanzoni mwa Oktoba.

Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Afya imewaondoa wasiwasi watanzania kuhusu uhaba  wa dawa nchini na kueleza kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 53.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Mpoki Ulisubisya amesema hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi mwanzoni mwa Oktoba.

Amesema kati ya dawa muhimu 135 zinazohitajika,ghalani zipo aina 71 na nyingine zipo kwenye vituo vya kutolea huduma.