Zaidi ya wagonjwa sita hufanyiwa upasuaji kila siku Kibondo

Muktasari:

Akizungumza na Mwananchi, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Adam Jonathan alisema kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa, watumishi katika hospitali hiyo wameanza kuzidiwa.

Kibondo. Imeelezwa kuwa kati ya wagonjwa sita hadi saba wanaofika kila siku katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma hufanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Mwananchi, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Adam Jonathan alisema kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa, watumishi katika hospitali hiyo wameanza kuzidiwa.

Dk Jonathan alisema nyakati za usiku wagonjwa huongezeka zaidi kwenye wodi za wanawake na watoto wakiwa na matatizo mbalimbali, wengi wao kutoka katika kambi za wakimbizi za Nduta iliyoko Kibondo na Mtendeli iliyoko wilayani Kakonko.

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Innocent Msilikale alisema tatizo la hospitali hiyo kulemewa na idadi kubwa ya wagonjwa ni kutokana na idadi ndogo ya watumishi wa afya waliopo ingawa baadhi ya mashirika ya kuhudumia wakimbizi yamepeleka watumishi ili kuongeza nguvu katika hospitali hiyo.