Zijue sababu za kufungwa biashara 2,000

Picha ya Mtandao

Muktasari:

  • Wadau hao wamependekeza kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na kuboreshwa kwa uhusiano kati ya wafanyabishara na Serikali.
  • Awali, taarifa ya utekelezaji wa bajeti kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ilibainisha kuwa kati ya Agosti na Oktoba, 2016 kulikuwa na wimbi la kufungwa biashara, ingawa alisema wizara haikupata sababu za wafanyabiashara  kuzifunga.

Dar es Salaam. Hali ya kufungwa kwa biashara 2,000 katika miji ya Dar es Salaam na Arusha imewaamsha wadau wa uchumi, ambao wameeleza kiini cha kuporomoka huko.

Wadau hao wamependekeza kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na kuboreshwa kwa uhusiano kati ya wafanyabishara na Serikali.

Awali, taarifa ya utekelezaji wa bajeti kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ilibainisha kuwa kati ya Agosti na Oktoba, 2016 kulikuwa na wimbi la kufungwa biashara, ingawa alisema wizara haikupata sababu za wafanyabiashara  kuzifunga.

Alisema Manispaa ya Ilala ilifunga biashara 1,076, Kinondoni (443), Temeke (222) na Arusha zilifungwa 131 na nyingi kati ya zilizofungwa ni za sekta za ujenzi, biashara za jumla, rejareja na huduma za usafiri.