Mwandishi mkongwe Kenya apigwa risasi ya tumbo

Muktasari:

Gullman, mzaliwa wa Italia aliyeishi Kenya kwa zaidi ya 30 alipigwa risasi na watu hao akiwa shambani kwake, huko Laikipia.

Nairobi. Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa watu wasiofahamika wamempiga risasi ya tumbo Mwandishi maarufu wa nchini Kenya, Kuki Gullman.

Gullman, mzaliwa wa Italia aliyeishi Kenya kwa zaidi ya 30 alipigwa risasi na watu hao akiwa shambani kwake, huko Laikipia.

Gazeti la The Star la nchini humo linaeleza kuwa mwezi uliopita mkahawa wake wa kifahari wa Mukuta uliteketezwa  kwa moto na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji.

Gallmann anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake 'I Dreamed of Africa'.

Filamu ya kitabu hicho pia ilitolewa, mhusika mkuu, akiwa mwigizaji maarufu wa Marekani , Kim Basinger.

 Tutaendelea kukujuza kuhusu habari hii.