Atuhumiwa kumkata panga mtoto wa kakaye

Muktasari:

Tukio hilo lilitokea Julai 27 saa kumi na moja jioni katika Mwalo wa Igombe.

Mwanza. Mvuvi mmoja, mkazi wa Kata ya Bugogwa, Wilaya ya Ilemela mkoani hapa, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wa kaka yake, Samwel Zozo (16) kwa kumcharanga kwa panga akidai amemwibia mafuta na samaki kwenye  mitumbwi yake.

Tukio hilo lilitokea Julai 27 saa kumi na moja jioni katika Mwalo wa Igombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema juzi kuwa: “Sijapata taarifa kama mtuhumiwa huyo amepatikana, hivyo tunaendelea kumtafuta ili afikishwe mahakamani.”