Watakiwa kuhoji matumizi ya fedha

Muktasari:

Mratibu wa mafunzo ya ufuatiliaji wa bajeti ya Serikali yanayoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Geofrey Chambuwa alisema jana kuwa, fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii lakini hazitumiki kwa malengo yaliyokusudiwa.

Morogoro. Wakazi wa Wilaya ya Morogoro wametakiwa kufuatilia na kuhoji matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Mratibu wa mafunzo ya ufuatiliaji wa bajeti ya Serikali yanayoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Geofrey Chambuwa alisema jana kuwa, fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii lakini hazitumiki kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Kuna sekta zinazokabiliwa na changamoto kubwa zikiwamo za maji, afya na elimu, ni vyema mkafuatilia ili zitumike kikamilifu,” alisema Chambuwa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kisaki, Paschal Lucas alisema: “Madiwani wanajadili mambo mengi katika vikao vya baraza lakini hawawajibiki moja kwa moja kutuletea taarifa hali inayosababisha tuone miradi ikitekelezwa katika maeneo yetu wakati hatuna tunalolijua.”