Waziri Mwijage asema maonyesho ya Sabasaba yamekidhi viwango
Muktasari:
Ameyasema hayo leo Julai 4 wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika maonyesho hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa hotuba yake.
Dar es Salaam.Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Wafanyabiashara yamekidhi viwango vya DITF kwani yamewahusisha Wafanyabiashara wazawa na wa kimataifa.
Ameyasema hayo leo Julai 4 wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika maonyesho hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa hotuba yake.
Mwijage amesema maonyesho hayo yamehudhuriwa na wafanyabiashara wa ndani 2900 na a nje 2500 na nchi 33.
"Maonyesho haya yamekidhi viwango vya Maonyesho ya Kimataifa ya Wafanyabiashara (DITF) na walioshiriki maonyesho hayo wanaonyesha bidhaa ambazo zimetengenezwa hapa nchini kupitia iwanda vyetu" amesema.