Waziri Mkuu azindua maonyesho ya Sabasaba
Muktasari:
Majaliwa ameyasema hayo leo Julai 4 na kuwakumbusha wafanyabiashara kuwa kuna maonyesho ya karne ya 21 yatakayofanyika China Septemba mwaka huu.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi maonyesho ya biashara ya kimataifa, maarufu Sabasaba huku akiwataka wafanyabiashara nchini kutumia fursa hiyo ili kutangaza bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.
Majaliwa ameyasema hayo leo Julai 4 na kuwakumbusha wafanyabiashara kuwa kuna maonyesho ya karne ya 21 yatakayofanyika China Septemba mwaka huu.
"Naomba maonyesho haya watanzania tushiriki kwa wingi na siyo haya tu maonyesho yoyote yale yanayofanyika nchi mbalimbali tunapaswa kushiriki ili kutangaza bidhaa zetu na kukuza soko la bidhaa za Tanzania,"amesema.
Pia amewataka Wafanyabiashara waliotoka mataifa mbalimbali hapa nchini kuendelea kuja kuonyesha bidhaa zao ili watanzanai wajifunze pia kupitia kazi zao na wao wajifunze vitu vinavyotengenezwa na watanzanaia.
Pia amewataka wafanyabiashara kutumia maonyesho ya sababsa kuwa sehemu ya kutafuta fursa kutoka nje ya nchini.