Waziri wa Fedha alia na wafanyabiashara wadanganyifu

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango.

Muktasari:

Akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Kigoma juzi, aliwataka wafanyabiashara kuacha udanganyifu katika ulipaji kodi kwa kuwa Taifa halipaswi kuendelea kutegemea misaada kutoka kwa wahisani ambayo kuifanya nchi kushindwa kufanya uamuzi sahihi.

Kigoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amewataka wafanyabiashara kulipa kodi ili lengo la makusanyo ya ndani lifikiwe kuepuka kutegemea wahisani ambao hutoa fedha zao kwa masharti.

Akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Kigoma juzi, aliwataka wafanyabiashara kuacha udanganyifu katika ulipaji kodi kwa kuwa Taifa halipaswi kuendelea kutegemea misaada kutoka kwa wahisani ambayo kuifanya nchi kushindwa kufanya uamuzi sahihi.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani hapa, Raymond Ndagiye alisema wako tayari kuunga mkono juhudi hizo endapo kodi itapunguzwa kwa kujali kipato cha wafanyabiashara.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alisema makusanyo yapo kwa màkusudi au malengo na kodi hulipwa ili kukuza kipato cha manispaa na wananchi wake.